top of page
Makala za Mwanadikala


JE, TISS INAHUSIKA KWELI? Uchambuzi wa Kiitelijensia Kuhusu Tukio la Nyumbani Kwa John Heche
Na. Rev. Godwin Chilewa Katika mazingira ya kisiasa yenye joto, matukio yasiyoeleweka mara nyingi hugeuzwa haraka kuwa ushahidi wa njama kubwa. Tukio la gari jeupe lililoripotiwa kuonekana likiulizia na hatimaye kufika nyumbani kwa John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, limezua mjadala mkali. Wapo waliokimbilia kuhusisha TISS na kile kinachodaiwa kuwa jaribio la kumdhuru mwanasiasa huyo. Hata hivyo, uchambuzi wa kitaalamu wa kiintelijensiau unaonesha kuwa hitimisho hilo li
1 day ago


UGAIDI AU SIASA ZA HOFU? Uchambuzi wa Kiitelijensia Kuhusu Mkakati wa Serikali Katika Kudhibiti Maandamano Nchini
Rev. Godwin Chilewa Hivi sasa kuna mwelekeo unaotia mashaka kwa jinsi serikali inavyoshughulikia maandamano ya raia na upinzani wa kisiasa. Hatua iliyochukuliwa hivi karibuni ya kuwakamata watu zaidi ya 130, wakiwemo wasomi kama muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma, na kuwafungulia mashtaka ya ugaidi, imezua taharuki na mjadala mpana kuhusu usalama wa taifa na uhuru wa kiraia. Watu wengi ikiwa pamoja na wanasheria na wanasiasa wakongwe wanajiuliza kama mkakati huu unasaidia kul
3 days ago


NCHIMBI, SAUTI YA MAGEUZI AU MBINU YA KISIASA? Uchambuzi wa Kiitelijensia Juu ya Hotuba ya Julai 24, 2026
Katika siasa, kuna nyakati ambazo kauli ya kiongozi hubeba taswira mbili. Huwa mawasiliano ya kawaida ya umma, na pia operesheni ya kimkakati inayolenga kudhibiti mwelekeo wa fikra za jamii, kupunguza shinikizo la kisiasa, na kulinda uhalali wa mfumo uliopo. Hotuba ya Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi aliyoitoa tarehe 24 Julai 2026 mbele ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania inaingia moja kwa moja katika kundi hili la mawasiliano ya kimkakati. Ukiangalia kwa juu
Jul 24


ATCL na Ndoto ya Ndege Nane Mpya: Uwekezaji wa Kimkakati au Kuendelea Kufadhili Hasara?
Na. Rev. Godwin Chilewa Nianze kwa kuweka angalizo kwamba makala hii haijadili kama Tanzania inahitaji shirika la Ndege, bali kama njia inayotumika kuliendesha ina mantiki kiuchumi? Kwa maana uhitaji wa shirika la ndege ni suala moja na mchakato wa kuliendesha ni suala lingine. Uamuzi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuongeza ndege nane ifikapo mwaka 2030 umeibua mjadala mpana kuhusu uhalali wa kuendelea kuwekeza fedha nyingi za umma katika sekta ya anga wakati shirika
Jul 23


KESI YA TUNDU LISSU: Siasa, Usalama, na Mustakabali wa Tanzania
Na Rev. Godwin Chilewa Katika historia ya siasa za Tanzania, kumekuwa na nyakati chache sana ambazo kesi ya mtu mmoja imebeba uzito mkubwa kiasi cha kuathiri mwelekeo mzima wa taifa. Kesi ya Tundu Lissu ni mojawapo ya nyakati hizo. Kesi hii ni ya kipekee kisheria, na ni kioo kinachoakisi mvutano wa ndani wa mfumo wa kisiasa wa Tanzania kati ya udhibiti wa dola na wito wa mageuzi ya kidemokrasia. Tundu Lissu ni mwanasiasa wa aina yake katika uwanja wa siasa za Tanzania. Kwa z
Jul 23


TISS Isifanye Kosa Lililofanywa na CIA
Katika ulimwengu wa intelijensia, makosa makubwa hayaanzi na kutopatikana kwa taarifa bali kwa namna taarifa hizo zinavyotafsiriwa. Hivyo miongoni mwa makosa hatari zaidi ya kiitelijensia ni kile kinachoitwa confirmation bias. Hili ni tatizo la kisaikolojia linaloweza kuyumbisha maamuzi ya kitaifa na hata kusababisha majanga ya kisiasa, umwagaji damu, na migogoro ya kidiplomasia. Confirmation bias ni hali ambapo mchambuzi wa idara ya usalama au taasisi huchagua, kuamini, au k
Jul 18


URITHI WA MADARAKA AU DEMOKRASIA?
Na Rev. Godwin Chilewa Kifo cha ghafla cha Seneta mashuhuri wa Marekani, Lindsey Graham, kimeacha gumzo kubwa kisiasa kwa sababu ya pengo la uongozi wake, Hata hivyo hatua ya dada yake, Darline Graham Nordone, kuchukua nafasi yake katika Seneti imewaacha hoi hata wale waliozoea kupora madaraka! Wengi wanajiuliza kama huu ni urithi wa kisiasa? Au ni utekelezaji halali wa sheria? na kama ni utaratibu wa kisheria nini athari zake kwa mustakabali wa demokrasia, hasa kwa nchi za
Jul 16


Georgia Guidestones: Jiwe la Siri, Ajenda ya Dunia, au Tafsiri Iliyopotoshwa?
Je, umewahi kusikia habari za Georgia Guidestones, mnara wa mawe uliosimama kwa miongo kadhaa katika jimbo la Georgia, nchini Marekani? Wengi wa walioujua waliuita “Stonehenge ya Marekani,” wakiufananisha na ule mnara wa kale wa mawe uliopo nchini Uingereza. Lakini kwa wengine ulikuwa zaidi ya sanaa, ulikuwa ujumbe wa siri, ajenda ya dunia mpya, na mwongozo wa kizazi kijacho baada ya maangamizi. Mnara huu ulijengwa mwaka 1980 katika eneo la Elbert County. Jambo lililozua u
Jul 13
bottom of page


