KUTANA NA
GODWIN CHILEWA

Bw. Godwin Chilewa anao uzoefu wa hali ya juu katika masuala ya intelejensia, ulinzi na usalama. Alipokuwa mtumishi mwandamizi wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Godwin alifanya kazi na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa pamoja na idara ya Usalama wa Taifa (TISS), kikosi cha makomando wa JWTZ (92KJ) idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai (CID), na idara ya ukachelo ya Marekani (Federal Bureau of Investigation). Bw. Godwin amehitimu shahada ya saikolojia katika chuo kikuu cha Houston (University of Houston Downtown) na shahada ya Uzamili (MBA) kutoka DeVry University- Houston, Texas. Vitabu vyake vingine ni pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa – Ni Chombo Cha Mauaji? Shuhuda za Jasusi - Ndani ya Idara, na Tufani Inapovuma.
